Welcome to Command and Staff College

Chuo cha Ukamanda na Unadhimu (CSC)-Duluti, kilianzishwa mwaka 1979, miezi michache baada ya kumalizika kwa Vita vya Kegera, kikiwa na lengo la kuwavisha umahili Maafisa wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na nchi marafiki katika kutekeleza majukumu ya Ukamanda na Unadhimu.

Chuo hiki awali kilijengwa Fort Ikoma kwenye bonde la hifadhi ya mbuga ya Serengeti mkoani Mara; baadaye mwaka 1989 kikahamishiwa wilayani Monduli mkoani Arusha kikiwa sambamba na Chuo cha Taaluma cha Kijeshi (TMA). Mwaka 2015 kilihamishiwa Duluti nje kidogo ya jiji la Arusha ambapo ndio sehemu yake ya kudumu.

Kutokana na mabadiliko ya sayansi na tekenolojia pamoja na kuongezeka kwa vitisho vya usalama, Chuo kilimua kushirikiana na Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) kuanza kutoa elimu ya Stashahada na Stashahada ya Juu ya Masomo ya Mkakati wa Usalama (Strategic studies), ambayo hufundishwa sambamba na masomo ya csc.Baada ya kupata kibali (accreditantion) kutoka Mamlaka ya Elimu ya Ufundi na Ufundi Stadi (NACTVET) mwaka 2020, kwa sasa Chuo kinafundisha masomo ya Ulinzi na Usalama (Defence and Security Studies) katika ngazi ya Stashahada na Shahada ya Uzamili bila kushirikiana na Chuo kingine kuanzia mwaka 2021.