KANALI KHAJI MAULID MTENGELA
Administration Title MKUFUNZI MKUU NA NAIBU MKUU WA CHUO

WASIFU

Kanali Khaji Maulid Mtengela aliteuliwa kuwa Mkufunzi Mkuu na Naibu Mkuu wa Chuo mwaka 2021. Alijiunga na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania Machi 01, 1995 baada ya kuhitimu Mafunzo ya Awali ya Kijeshi. Alihudhuria Kozi ya Afisa Mwanafunzi katika Chuo cha Maafisa Wanafunzi Monduli (TMA) na kupata Kamisheni Mei 24, 1997 na kutunukiwa cheo cha Luteni Usu.

Baada ya Kamisheni alihudhuria Kozi mbalimbali ndani na nje ya nchi ifuatavyo:-

 • "Comparative Course” (CSC), mwaka 2016 nchini Ghana;
 • Semina ya Ukufunzi, mwaka 2015 nchini Tanzania;
 • Kozi ya Ukamanda na Unadhimu (CSC), mwaka 2014 nchini Tanzania;
 • Kozi ya Uongozi wa Kombania ya Vifaru, mwaka 2008 nchini China;
 • Kozi ya Ulinzi wa Amani, mwaka 2007 nchini Namibia;
 • Kozi ya Uongozi wa Kombania, mwaka 2006 TMA;
 • Kozi ya Ungozi wa Patuni, mwaka 1999 nchini Tanzania; Aidha, kabla ya kuteuliwa kushika madaraka ya Mkufunzi Mkuu na Naibu Mkuu wa Chuo, ameshika nyadhifa mbalimbali ndani ya JWTZ na nje ya Jeshi ifuatavyo:-
 • Mnadhimu Elekezi wa mpango wa Kubadilishana (DS on Exchange Programme) CSC nchini Rwanda;
 • Mnadhimu Elekezi CSC – Tanzania;
 • Kamanda Kombania;
 • Mkufunzi wa Shule ya Vifaru;
 • Afisa Utawala; na
 • Kamanda Kombania ya Vifaru.

Vile vile ametunukiwa Medali ifuatavyo:-

 • Medali ya Utumishi Uliotukuka;
 • Medali ya Utumishi Mrefu;
 • Medali ya Miaka 50 ya Uhuru;
 • Medali ya Miaka 50 ya Muungano;
 • Medali ya Miaka 50 ya JWTZ;
 • Medali ya Comoro na Anjuan;
Medali ya Miaka 40 ya JWTZ;