Brigedia Jenerali Sylvester Ghuliku
Administration Title Kaimu Mkuu wa Chuo

WASIFU WA BRIGEDIA JENERALI SYLVESTER GHULIKU (MKUU WA CHUO)

Brigedia Jenerali Sylvester Ghuliku ni Mkuu wa Chuo wa kumi na saba kukiongoza Chuo cha Ukamanda na Unadhimu – Duluti Tanzania tangu alipoteuliwa kushika madaraka hayo tarehe 30 Juni 2020.

Brigedia Jenerali Sylvester Ghuliku alijiunga na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania tarehe 19 Juni 1998 na kuhudhuria Kozi ya Afisa Mwanafunzi na kupata Kamisheni mwaka 2000 kuwa Luteni Usu.

Brigedia Jenerali Sylvester Ghuliku amehudhuria kozi mbalimbali nchini Tanzania, Afrika Kusini na Zimbabwe.

Brigedia Jenerali Sylvester Ghuliku katika kulitumikia Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania kabla ya kuwa Mkuu wa Chuo ameshika nyadhifa mbalimbali zikiwemo Mhandisi Usanifu na Matengenezo Nyumbu Project, Mnadhimu Mwelekezi Chuo cha Ukamanda na Unadhimu, Mkuu wa Shule ya Mafunzo ya Huduma, Mkurugenzi wa Uhandisi na Umeme Makao Makuu ya Jeshi, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa na Mkufunzi Mkuu Chuo cha Ukamanda na Unadhimu.

Brigedia Jenerali Sylvester Ghuliku ametunukiwa medali mbalimbali ifatavyo:-

  • Medali ya Utumishi Uliotukuka.
  • Medali ya Utumishi Mrefu.
  • Medali ya Miaka 50 ya Uhuru.
  • Medali ya Miaka 50 ya Muungano.
  • Medali ya Miaka 50 ya JWTZ.
  • Medali ya Comoro na Anjouan.
  • Medali ya Miaka 40 ya JWTZ.