Kanali KM MTENGELA
Administration Title Mkufunzi Mkuu

WASIFU WA KANALI KHAJI MAULID MTENGELA (MKUFUNZI MKUU)

Kanali Khaji Maulid Mtengela ni Mkufunzi Mkuu wa kumi na saba wa Chuo cha Ukamanda na Unadhimu – Duluti Tanzania tangu alipoteuliwa tarehe 30 Juni 2022 na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali, Jacob John Mkunda

Kanali Khaji Maulid Mtengela alijiunga na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania tarehe 30 March 1995 na kuhudhuria kozi ya afisa mwanafunzi na kupata kamisheni mwaka 1997 kuwa Luteni Usu.

Kanali Khaji Maulid Mtengela amehudhuria kozi mbalimbali nchini Tanzania, zikiwemo zilizoendeshwa katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Tanzania – Monduli na Chuo cha Ukamanda na Unadhimu – Monduli. .

Kanali Khaji Maulid Mtengela katika kulitumikia Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania ameshika nyadhifa mbalimbali zikiwemo Troop Comd 83 Regt 1999-2003, Sqn Comd 83 Regt 2003-2005, Adjuntant 83 Regt 2005-2012, Instructor 83 Regt 2008-2012 , District Reserve Force Advisor - Mkulanga 2013-2015, Directing Staff CSC 2015–2012 Duluti Tanzania Directing staff on exchange pgme Rwanda defence force CSC 2019-21,Mkufunzi mkuu Chuo cha Ukamanda na Unadhimu – Duluti Tanzania 2022 - Current )


Kanali Khaji Maulid Mtengela ametunukiwa medali mbalimbali ifuatavyo:-

  • Medali ya Utumishi Uliotukuka.
  • Medali ya utumishi Mrefu.
  • Medali ya miaka 50 ya Uhuru.
  • Medali ya miaka 50 ya Muungano.
  • Medali ya miaka 50 ya JWTZ.
  • Medali ya Comoro na Anjouan.
  • Medali ya miaka 40 ya JWTZ.